ZGPL

CHUONI WACHAPA 2 ZGPL

Na Mohammed Ally

Ligi kuu ya Zanzibar, maarufu Zanzibar Grand Malt Premier League, imemaliza mzunguko wake wa kwanza jana kwa kushudi mechi moja iliyochezwa katika uwanja wa Amaan ikiwakutanisha timu ya Chuoni na Mundu kutoka Kaskazini mwa kisiwa cha Unguja.

Mechi hiyo imemalizika kwa timu ya Chuoni kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, mabao ya Chuoni yote mawili yakifungwa kipindi cha kwanza kupitia kwa Shaffii Hassan katika dakika ya 44, bao la pili likifungwa na Ahmed Malik katika dakika ya 44, bao pekee la Mundu likipatikana katika kipindi cha pili cha mchezo mfungaji akiwa ni Mfanyeje Mussa katika dakika ya 56.

Itakumbukwa kuwa klabu ya Mundu ilikwishateremka daraja lakini wakanunua daraja kutoka kwa klabu ya Miembeni United.

Mzunguko wa pili wa ligi hiyo unatarajia kuendelea tena Jumamosi ijayo (15.09.2012) kwa michezo miwili, kisiwani Pemba katika uwanja wa Gombani.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo na wawakilishi wa Zanzibar katika ligi ya mabingwa barani Afrika, Super Falcon wakikipiga na Duma timu inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga chumi la Zanzibar (JKU).

Itakumbukwa kuwa mechi iliyopita Super Falcon walipoteza baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Chipukizi, huku Duma wakikubali kipigo kama hicho kutoka kwa wawakilishi wa Zanzibar katika kombe la shirikisho, timu ya Jamhuri.

Kisiwani Unguja katika uwanja wa Amaan mabaharia wa KMKM ambao walipoteza mchezo wao uliopita baada ya kukubali kipigo chembamba cha bao 1-0 kutoka kwa Mafunzo, watateremka uwanjani hapo kukabiliana na Malindi ambao nao katika mechi yao ya kwanza walipoteza dhidi ya Bandari baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-2.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.