HESABU ZA TFF ZAZIDI ZA SUPER SPORT

Shirikisho la mpira wa miguu la Tanzania 'TFF' leo wametangaza idadi ya watazamaji walokata tiketi katika mpambano wa jana (mei 18) wa watani wa jadi ambazo ni zaidi ya watu 121 kwa zile zilizotangazwa na super sport hapo jana.

Super sport wakiwa wanaonyesha mchezo huo namba 180 moja kwa moja walitangaza mahudhurio ya mashabiki katika mchezo huo kuwa 57,285 wakati TFF leo wamesema watazamaji walio kata tiketi wanafika 57,406 na kuingiza Tsh. 500,390,000.

Katika michezo ya nyuma takwimu zinazotolewaga na super sport katika michezo wanao rusha moja kwa moja toka katika uwanja wa Taifa huwa ni zaidi ya zile zinazotangazwa na TFF wakati wakitangaza mapato ya mchezo husika.

Katika mchezo wa jana uliomalizika kwa yanga kuwachapa simba goli 2-0, lilizipa kila klabu Tsh. 123,970,927.45 wakati ongezeko la thamani (VAT) likipelekwa Tsh. 76,330,677.97.

Kiingilio cha Tsh 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walio kata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza Tsh. 95,195,000 wakati kile cha Tsh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana Tsh. 123,515,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja Tsh. 63,036,064.81, tiketi Tsh. 3,818,890, gharama za mechi Tsh. 37,821,638.88.

Kamati ya Ligi Tsh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Tsh. 18,910,819.44 na chama cha mpira wa miguu cha Dar es salaam (DRFA) Tsh. 14,708,415.12.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.