wachezaji

MKUDE: NIOMBEENI DUA

http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/10/mkude.jpg
KIUNGO wa timu ya Simba, Jonas Mkude amewataka Wanasimba, kumuombea aweze kupona haraka, mkono wa kushoto alioumia katika mchezo wa juzi dhidi ya Yanga, uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mkude aliumia dakika za mwisho za mchezo huo, na kusababisha kutolewa nje akiwa kwenye machela, ambapo baada ya kutoka pengo la nyota huyo lilionekana kutokana na safu hiyo kuanza kupwaya tofauti na awali.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mkude alisema, aligongana na mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa, mpaka kupata maumivu makali yaliyosababisha hasiweze kurudi tena dimbani.
“Nimeumia sana, hapa mkono unaniuma mno, lakini naamini nitapona tu, tayari nimefungwa mabandeji ya kuinua mkono ila awali nilikuwa na maumivu makali sana,” alisema Mkude.

Mkude alirejea hivi karibuni dimbani, baada ya kuwa majeruhi takribani wiki nne na kucheza katika mchezo huo ambao awali ulikuwa uchezwe Oktoba 12 na kusogezwa mbele.


CHANZO: TANZANIA DAIMA

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.