vilabu

AZAM FC WAPATA SARE KWA ZESCO, DUMAYO AKIPIGA MBILI

Kiungo wa azam fc Franky Domayo leo ameifungia Azam fc goli 2 katika sare ya goli 2-2 dhidi ya mabingwa wa Zambia ZESCO United katika mchezo wa michuano maalum mifupi iliyoandaliwa na TP Mazembe ya DR Congo.

Katika mchezo huo ZESCO United waliuwanza mchezo kwa kasi wakicheza soka safi waliandika goli katika dakika ya 26, goli hilo liliwaamsha Azam fc na kuwarudisha mchezoni na kuanza kushambuliana kwa zamu.

Kazi nzuri ya Shomari Kapombe iliyomaliziwa vyema na Franky Domayo akiunga mpira aliotengewa na Didier Kavumbagu na kuipatia azam fc goli la kusawazisha katika dakika ya 42 na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa azam fc kuutawala mchezo na katika dakika ya 62 Franky Domayo aliiandikia Azam fc goli la 2, akiunga pasi ya Shomari Kapombe ambaye alipenyezewa vyema na Mudathir Yahya.

Katika dakika ya 75 ZESCO United walipata penati ambayo walifanikiwa kupata goli la kusawazisha na kupelekea mchezo kwisha kwa sare ya goli 2-2.

Katika mchezo wa kwanza leo katika michuano hiyo ya TP Mazembe ilishuhudia TP Mazembe wakiibuka na ushindi wa goli 3-1 walipo kuwa wanakabhliana na Don Bosco.

Michezo ya mwisho inatarajiwa kuchezwa februari 3 ambapo Azam fc watawakabili Don Bosco wakati TP Mazembe wakicheza na ZESCO United.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.