simba

SIMBA SC WASHINDWA KUZIONA NYAVU ZA JULIO

Mchezaji Mpya wa Simba SC aliyetokea
Azam FCkwa Mkopo Joseph Kimwaga
Mabingwa wa ligi daraja la kwanza Mwadui FC leo wametoa sare ya bila kufungana na Simba SC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Taifa leo jioni.

Katika mchezo wa leo Simba SC walikuwa wanampima mshambuliaji wao toka Senegal Niang huku wakimtumia kwa mara ya kwanza mchezaji wao mpya walio mchukuwa toka Azam FC kwa mkopo Joseph Kimwaga.

Simba SC walitengeneza nafasi kadhaa za kujipatia goli lakini waliishia kupoteza nafasi hizo, sambamba na Mwadui ambao walitengeneza nafasi chache na kushindwa kuzitumia nafasi hizo.

Kikosi cha Mwadui kinachonolewa na kocha Jamhuri Kihwelo Julio, kimiekuwa kikosi cha kwanza kuambulia sare kwa Simba SC inayonolewa na Muingereza Kerr.

Kabla ya Mchezo wa leo kikosi cha Kerr kilikuwa bado hakijaambulia sare wala kufungwa katika michezo aliyo kiongoza huku leo akiambulia sare ya kwanza dhidi ya kikosi kinachoundwa na wachezaji wengi walio wahi kutamba na Simba SC na Yanga.

Mshambuliaji wa zamani wa yanga Jerry Tegete aliichezea leo Mwadui mchezo wa pili toka ajiunge na timu hiyo yenye maskani yake mkoani Shinyanga.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.