simba

WALEWALE WAIMALIZA SIMBA SC, NA KUISHUSHA MPAKA NAFASI YA 3


Wauwaji wale wale wa mchezo wa kwanza walipokutana Simba na yanga, na leo hii wanawamaliza Simba SC kwa goli 2-0, kartika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa leo ambao Simba SC kwa takribani dakika 66 walicheza wakiwa pungufu baada ya beki wake Abdi Banda kuzawadiwa kadi nyekundu katika dsakika ya 23 ya mchezo ikiwa ni baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Yanga sc waliuwanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya kwanza kama mpigaji wa faulo angeipiga vyema yanga wangeandika goli la kwanza lakini mpira wake uliishia mikononi mwa kipa Vicent Agban.

Baada ya kosa kosa hiyo Simba SC nao walijibu pigo na kuendelea kushambuliana kwa zamu kwa dakika 23 za mwanzo kabla ya Banda kupewa kadi nyekundu.

Yanga SC waliandika goli la kwanza katika dakika ya 39 kupitia kwa Donald Ngoma ambaye aliwahi mpira ambao Hassan Kessi aliurejesha kwa kipa na mpira kuwa mfupi na kupelekea Ngoma kumchambua kipa na kuiandikia Yanga goli la uongozi.

Goli hilo lilpeleka Yanga kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0, na katika kipindi cha pili Simba SC walijaribu kusaka goli la kusawazisha bila mafanikio.

Katika dakika ya 71 Amisi Tambwe akiungfa krosi ya mtokea benchi Geofrey Mwashiuya na kuiandikia yanga goli la pili, goli lililo imaliza Simba SC na kupelekea kupoteza mchezo kwa kukubali kufungwa goli 2-0 na yanga.

Ushindi huo wa pili msimu huu Yanga SC wanaupata mbele ya Simba SC unaifanya Simba SC kushuka mpaka nafasi ya tatu huku Yanga ikirejea kilelelni na Azam FC wakishika nafasi ya pili.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.