VPL

KAGERA SUGAR YAICHAPA JKT RUVU

Wakatamiwa wa Misenye mkoani Kagera, Kagera Sugar leo wamefanikiwa kuifunga JKT Ruvu, katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.

Katika mchezo huo wa leo Kagera sugar wameibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililo fungwa na Mbaraka Yusuph, na kuipa pointi tatu muhimu Kagera sugar hii leo.

Ligi kuu ya vodacom inataraji kuendelea kesho kwa michezo sita kuchezwa ambapo Azam Fc watawakaribisha Mtibwa sugar mchezo utakaochezwa saa moja usiku katika uwanja wa Azam complex.

Yanga SC watakuwa wa geni wa Toto Afrika katika uwanja wa CCM Kirumba, Ruvu shooting watakuwa wenyeji wa Mwadui katika uwanja wa Mabatini, Ndanda FC wakiwakaribisha Mbeya City, huku Stand wakiwa wageni wa Tanzania Prisons.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.