CHAMA cha Netiboli Tanzania (CHANETA) kimeitaka mikoa iliyothibitisha ushiriki wao kwenye mashindano ya kombe la Taifa kufanya hivyo kwa maandishi na sio kwa mdomo kama ambavyo wengi wamefanya hivyo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Chaneta, Anna Kibira alisema mikoa mingi iliyothibitisha imesema kwa mdomo pasipo kujibu kwa maandishi kwenye barua pepe, jambo linalotia shaka dhidi ya walichokisema kwani wasiposhiriki ni vigumu kuwabana.
Mashindano ya Kombe la Taifa yanatarajiwa kushirikisha mikoa 29 ya Tanzania bara ambapo hadi sasa timu zilizothibitisha kwa maneno ni 12, huku mikoa mingine ikiendelea kusubiriwa hadi mwisho wa kuthibitisha ambapo ni kesho na michunao hiyo imepangwa kufanyika Desemba 28.
“Tunahimiza mikoa yote iliyothibitisha ushiriki kwa mdomo wathibitishe tena kwa maandishi, watume kwenye barua pepe yetu, tutambue kweli watakuja kwenye mashindano na sisi inakuwa rahisi kuweka kwenye ratiba zetu kuwa nani na nani atakuwepo,”alisema.
Kwa mujibu wa Kibira, mikoa iliyothibitisha ushiriki kwa mdomo ni Arusha, Kagera, Shinyanga, Ruvuma, Mwanza, Kinondoni na Morogoro.
Aidha, bado ameendelea kuhimiza kampuni, taasisi na mashirika kujitokeza kuwasaidia ili kukamilisha mashindano hayo. Kibira alisema mashindano hayo ni muhimu kwa vile yatawezesha kuchagua wachezaji wenye uwezo wa kuingia kwenye timu ya Taifa.
CHANZO: HABARI LEO

0 comments:
Post a Comment