Mimi

Sports In Bongo (SIB) ni blog inayokuletea taarifa za michezo mbalimbali inayojiri Tanzania. Hapo awali ilikuwa inatoa taarifa za mpira wa miguu (Kandanda) pekee na ilikuwa ina kwenda kwa jina la Aboodmsuni na Soka la Bongo likiwa ni jina la pili toka kwa lile la mwanzo ambalo ni Tanzania Football Event (TFE).

Blog hii ilianza kufanya kazi februari 21 mwaka 2011, ikitambulika kwa jina la Tanzania Football Event, ikiwa na dhamira ya kuripoti na kuzungumzia mpira wa Tanzania kuanzia kwenye ligi ndogo za mchangani mpaka ligi kuu Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Mnamo Machi mosi mwaka 2012, ilianza rasmi kuzungumzia michezo mingine na Machi 9, ikaanza kutambulika kwa jina la Sports In Bongo.

Katika blog hii utapata kinachojiri katika soka na michezo mingine (mpira wa kikapu, ngumi, judo, mpira wa neti, gofu n.k) inayojiri katika mipaka ya Tanzania na kidogo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, huku ukipata vichwa vya habari katika anga za kimataifa pamoja na video za matukio mbalimbali uwanjani na ratiba ya michezo mbalimbali zinazohusisha timu za Tanzania.


MAFANIKIO
Sports In Bongo ikiwa inatambulika kwa jina la Aboodmsuni Na Soka La Bongo ikiwa na miezi mitano tangu ianze kazi yake iliingizwa kwenye mashindano ya Tanzania Best blog 2011, katika kipengele cha best sport blog 2011 na kufanikiwa kuwa second runner.


LENGO

LENGO letu ni kuhakikisha tunatoa taarifa za michezo yote ndani ya mda muwafaka. Na ili kufikia lengo hili tunataraji kupata ushirikiano mzuri toka kwa wadau wa michezo husika.


MMILIKI

Sports In Bongo inamilikiwa na ABOODMSUNI NETWORK ambayo iko chini ya Abdallah Hamdun Ibrahim Sulayman.


WASILIANA NASI.

Unaweza kututumia habari yoyote kuhusu michezo ya Tanzania ama stori ya maisha ya mwanamichezo yoyote wa Kitanzania ama mawazo ya kuboresha habari zetu au ratiba na matokeo ya michezo katika anuani ya barua pepe ya aboodmsuni@gmail.com ama katika whatsapp +255 715 602 531 nasi tutaipachika ama kuifanyia kazi bila matatizo.



Je una matangazo na unataka kutangaza nasi, basi wasiliana nasi kupitia barua pepe ya aboodmsuni@gmail.com


MAWASILIANO MENGINE.
Simu namba; +255 765 578 851, +255 715 602 531, +255 785 831 252, +255 625 510 161 ama +255 776 149 188
Barua pepe; aboodmsuni@gmail.com
Powered by Blogger.