MIYEYUSHO KUZIPIGA NA MKENYA


BONDIA Francis Miyeyusho, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano lake dhidi ya Mkenya, David Chalanga, litakalofanyika Ukumbi wa Msasani Club jijini Dar es Salaam, Desemba 31.

Mabondia hao wanaotamba Afrika Mashariki, watafunga mwaka kwa pambano hilo ambalo litakuwa la kuwania kugombea mikanda mikubwa ya ubingwa na kujiongezea rekodi ya ushindi.

Akizungumzia maandalizi ya pambano hilo, Miyeyusho alisema, yuko fiti wakati wowote, kwani hata sasa hivi kama mpinzani wake yuko tayari yeye yupo kwa ajili ya kupigana.

Pambano hilo litasindikizwa na ya utangulizi, ambapo Idd Mnyeke ataonyeshana ubabe na Cosmas Cheka, Anthony Mathias atazipiga na Fadhili Majia huku Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ akioneshana kazi na Mohamed Kashinde.

Katika pambano hilo, kutauzwa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile Manny Paquaio, Saul ‘Canelo’ Alverez, Floyd Mayweather, Mike Tyson, Muhamad Ali, Ferex Trinidad na Miguel Cotto.

Pia kutakuwa na vifaa vya mchezo huo vitakavyokuwa vikitolewa na kocha wa mchezo huo, Rajabu Mhamila ‘Super D’ kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa ngumi.


CHANZO: TANZANIA DAIMA

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.