YANGA, AZAM KUKUTANA MAPINDUZI CUP

Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi Azam FC na mabingwa wa Tanzania bara Yanga wamewekwa kwenye kundi moja katika michuano ya kombe la mapinduzi linalo tarajia kuanza januari 1 mpaka januari 13 mwakani.

Azam na Yanga wamewekwa kwenye kundi C samabamba na Tusker ya Kenya na Kombaini ya Unguja, huku Simba SC wakiwa katika kundi B pamoja na AFC Leopards ya Kenya, KMKM na KCC ya Uganda. Wakati kundi A linaundwa na timu za Mbeya City, kombaini ya Pemba, Chuoni na URA ya Uganda.

Simba SC watafungua na AFC Leopads siku ya january mosi kuanzia saa 2 usiku, huku Januari 2 kukiwa na michezo minne katika viwanja vya Amani Unguja na uwanja wa Gombani Pemba.

Katika uwanja wa Amaan, Azam FC wataonyeshana kazi na Unguja Combine kuanzi saa 10:00 alasiri ukifuatiwa na mchezo kati ya Yanga na Tusker itakayorindima kuanzia saa 2:00 usiku.

Na katika uweanja wa Gombani shughuli itakuwa kati ya URA na Chuoni (kundi A) watakaovaana saa 8:00 mchana, huku Mbeya City ikitoana jasho na Pemba Combine, saa 10:00 jioni katika mchezo wa kundi A.


KUNDI A:
URA (Uganda)
Chuoni
Mbeya City
Pemba Combine

KUNDI B:
SImba SC
AFC Leopard (Kenya)
KMKM
KCC (Uganda)

KUNDI C:
Yanga SC
Azam FC
Tusker (Kenya)
Kombaini ya Unguja

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.