Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga wamejikuta wakipangiwa na bingwa wa Afrika El-Ahly katika raundi ya kwanza ya michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika hapo mwakani.
Yanga kabla ya kucheza na EL-Ahly wanatakuwa na kibarua cha kuhakikisha wanaiondosha michuanoni Komorozine ya Comoro katika hatua ya awali ambapo Yanga wataanzia nyumbani.
Wakati wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azam FC wamepangwa kucheza na Ferroviario Da Beira ya Msumbiji katika Raundi ya Awali na endapo wakifanikiwa kuwatoa watacheza na mshindi kati ya St. Michel ya Shelisheli na ASSM Elgeco Plus ya Madagacar.
Azam FC na Yanga wataanzia nyumbani katika mchezo wake wa raundi ya awali utakao chezwa kati ya february 7,8 na 9 wakati marejeano itakuwa kati ya februari 14,15 na 16 mwakani.

0 comments:
Post a Comment