TUZO ZA MABONDIA SASA JAN 25

ZILE tuzo za mabondia na waandishi wa habari waliofanya vema mwaka
2013 sasa zinatarajiwa kutolewa jijini Dar es Salaam, Januari 25.

Awali tuzo hizo zilikuwa zitolewe Desemba 28 mwaka jana, lakini
kutokana na maandalizi kutokamilika zikaahirishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari
(Maelezo), jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Said Msanga,
alisema utoaji wa tuzo hizo utafanyika Ukumbi wa PTA Sabasaba kuanzia
saa 12 jioni hadi 6 usiku.

"Tumechelewa kupata wadhamini mapema, tuliwapata PSPF wiki moja kabla
ya tukio kufanyika, tukaona hatutotenda haki kwani hawataweza
kujitangaza vizuri zaidi na ndiyo maana tukapeleka mbele hafla hii
ambayo ilitakiwa ifanyike tangu Desemba 28 mwaka jana," alisema
Msanga.

Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa BFT, Salum Viduka alisema
mchakato wa kumpata rais wa shirikisho hilo unaendelea vizuri licha ya
watu wengi bado hawajachukua fomu za kugombea.

"Mpaka sasa hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu, kutokana na kiwango
cha pesa tulichokiweka cha sh 300,000 na tumeamua kupandisha ili
tupate viongozi wenye nia thabiti," alisema.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.