TIMU YA UFUKWENI ZANZIBAR YAALIKWA KENYA


Chama cha soka Zanzibar (ZFA) kupitia kamati yake ya mpito wamepokea barua ya mualiko kutoka kwenye kamati ya mashindano ya soka la ufukweni nchini Kenya kwa kuwataka kushiriki kwenye mashindano yatakoyofanyika December 16 hadi 20 kwenye fukwe za Buntwani, kata ya Kilifi, Mji wa Malindi nchini Kenya.

Taarifa hiyo ameitoa afisa habari wa kamati ya mpito ZFA Ali Bakar Cheupe.

“Tumepokea mualiko huo kwa moyo mmoja na tunaamini ziara ya timu ya taifa ya Uganda ya soka la Ufukweni kuja hapa visiwani imetusaidia tukapatiwa mualiko” Alisema Cheupe.

Katika mashindano hayo kila timu inatakiwa ilipe gharama za usajili (Registration fee) ambayo ni shilingi 5000 za Kenya au dola 50 za kimarekani.

Mbali na gharama hiyo ya usajili timu inatakiwa ijilipie yenyewe gharama za usafiri wa kwenda na kurudi nchini humo.

Kwa upande wa kamati ya mashindano ambayo inaoongozwa na Madam Melda Munyazi itatoa huduma za chakula, malazi, usafiri na huduma nyingine zinazohusiana na mashindano hayo ambapo timu zinatakiwa kutibitisha ushiriki wake si zaidi ya tarehe 20 ya mwezi huu lakini pia tarehe ya mwisho ya usajili ni Novemba 30, 2015.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.