AJIBU, BOCCO WAPELEKA SARE MSIMBAZI NA CHAMANZI


Magoli ya John Bocco na Ibrahim Ajibu yametosha kupelekea Simba na Azam FC kugawana pointi hii leo katika mchezo wao wa 10 wa ligi kuu ya vodacom huku Satnd united ikikubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa Mwadui FC.

Katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa hii leo jijini Dar es salaam Azam FC walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa John Bocco akimalizia pasi safi ya Farid Mussa Maliki katika dakika ya kwanza ya mchezo.


Kuingia kwa goli hilo kulipelekea Simba SC kuamka na kuanza kucheza mpira huku Azam FC wakicheza taratibu wakionekana kuridhika kwa goli hilo.

Katika dakika ya 23 Ibrahim Ajibu aliiandikia Simba SC goli la kusawazisha akimalizia kazi nzuri ya Said Khamis Ndemla na Mohammed Hussein.

Katika kuelekea mapumziko Simba Sc walipoteza nafasio kadhaa kama ilivyo kwa Azam FC kabla ya goli la Hajjibu.

Kipindi cha pili kilianza tarartibu kila upande wakicheza kwa tahadhari zaidi, hiku wakiendelea kupoteza nafasi ya kujipatia goli la pili.

Simba SC waliandika goli la pili kupitia kwa Ibrahim Ajibu katika dakika ya 65 kabla ya John Bocco kuandika goli la pili kwa Azam FC katika dakika ya 74 na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.

Katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga Stand unityed walikubali kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa jirani zao Mwadui FC.

Magoli ya Mwadui FC yalifungwa na Fabian Ngaswe na Paul Nonga na kupatia ushindi wa tanokatika michezo 11 ya ligi kuu ya vodacom.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.