
Kocha mkuu wa City, Abdul Mingange ameuambia mtandao huu kuwa anarejea Mbeya akiwa na matumaini tele ya kuibuka mshindi kwenye mchezo wa jumamosi kufuatia matokeo mazuri kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Njombe Mji kwenye uwanja Halmashauri mjini Makambako ambapo vijana wake waliibuka na ushindi wa kwa bao 4-0.
“Jana tulicheza na Njombe Mji, huu ulikuwa ni mchezo muhimu kwangu kupima uelewano wa nyota wa safu yetu ya ushambuliji,hilo ndiyo lilikuwa jambo kubwa kwangu kwa sababu tulimaliza dakika 90 tukiwa na bao 4 huku wapinzani wetu Njombe Mji wakiwa bila bao lolote,nilifaarijika sana kwa sababu walinionyesha kuwa wameiva na wako tayari kuisambaratisha Mtibwa jumamosi, hivyo tunarejea Mbeya kwa ajili ya kazi moja tu”,alisema.
Huu utakuwa mchezo wa tano kwa timu hizi kukutana katika kinyang’anyiro cha ligi kuu ya Vodacom huku timu zote zikiwa zimeshinda mara moja na kutoka sare mara mbili katika misimu miwili iliyopita.
0 comments:
Post a Comment