SIMBA YAKANUSHA KUHUJUMIWA KUELEKEA KUIKABILI AZAM FC

Klabu ya Simba inapenda kutoa taarifa ya kukanusha habari zilizoandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari juu ya kuwepo hujuma ndani ya klabu hyo kuelekea mchezo wetu wa jumamosi dhidi ya timu ya Azam.

Taarifa hyo ni upuuzi na ina lengo la kuibua mgogoro ndani ya klabu na inajielekeza kututoa mchezoni kwenye mechi hiyo muhimu ya ligi kuu ya vodacom.

Kwenye taarifa hiyo ambayo imemnukuu rais wa Simba kuwa eti na yeye amezisikia taarifa hizo.na huku kukiwa hakuna chombo kilichoongea nae kuhusu jambo hilo.

Klabu ya Simba inawaomba wanachama na washabiki wetu sio tu kuzipuuza bali kuwa macho na maadui wa klabu ambao siku zote huibua mambo ya kutunga kwa nia ovu dhidi ya timu yenu.

Marajio yetu tunategemea vyombo vilivyoandika taarifa hizo kukanusha vikali uongo huo unaoshusha heshima ya vyombo hivyo.

Imetolewa na Haji Manara
Mkuu wa habari wa klabu ya Simba
Simba nguvu moja

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.