![]() |
Samatta |
Na
Prince Akbar
MBWANA Samatta amefunga bao moja jioni kwenye Uwanja wa TP
Mazembe mjini Lubumbashi, wakati timu yake Tout Puissant Mazembe ikiilaza Al
Ahly mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Samatta alifunga bao hilo dakika ya 49, baada ya
pasi nzuri ya Tressor Mabi Mputu, kabla ya D. Kanda kufunga la pili dakika ya 61,
pasi ya Mputu tena. Thomas Ulimwengu aliingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya
Kanda.
Mbwana ni mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha
Mazembe kwa mwaka wa pili sasa, lakini Ulimwengu alipandishwa kikosi hicho kwa
mara ya kwanza mwezi uliopita, baada ya kukaa kikosi cha wachezaji wa akiba
tangu asajiliwe katikati ya mwaka jana na leo amecheza mechi ya kwanza.
Mazembe imefikisha pointi10, baada ya kucheza mechi tano,
kushinda tatu, sare moja na Berekum Chelsea na kufungwa moja na Al Ahly ugenini,
Al Ahly iliyotoa sare ya 1-1 na Berekum Chelsea
nchini Ghana katika mechi yake iliyopita, bado inaongoza kundi hilo kwa pointi
zake 10, wakati wababe wapya wa Ghana wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao
sita baada ya kutoka sare na Zamalek 1-1, ambao wanashika mkia wakiwa na pointi moja.
Sasa Ahly na TPM zinawania uongozi wa kundi ili kujihakikishia kutinga Nusu Fainali kabla ya mechi za mwisho za Kundi hilo, ambazo Ahly watamaliza na Zamalek Cairo na Mazembe watamaliza Berekum Chelsea nchini Ghana
AKUFFO APIGA GOLI SIMBA WAKITOA SARE
Akuffo |
SIMBA SC imelazimishwa sare ya 1-1 na City Stars ya Nairobi Uwanja
wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha jioni hii, katika mchezo wa kirafiki
kujiandaa na mechi ya Ngao ya jamii dhidi ya Azam FC, Septemba 11, mwaka huu,
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Simba imeshindwa kulipa kisasi cha Agosti
8, mwaka huu ilipochapwa mabao 3-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na timu hiyo.
Katika mchezo huo, bao la Simba lilifungwa na Daniel Akuffo,
wakati Komabil Keita alijifunga katika jitihada za kuokoa na kuwapa Wakenya bao
la kuongoza.
Awali, Simba ilicheza mechi mbili Arusha, dhidi ya Mathare
United ya Kenya na JKT Oljoro ya Arusha, ambazo zote ilishinda 2-1,
mshambuliaji mpya Daniel Akuffo kutoka Ghana akifunga bao moja kila mechi,
Kiggi Makaasy na Mrisho Ngassa wakifunga mabao mengine.
Simba inajiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 11, mwaka
huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambayo kihistoria hiyo itakuwa mechi ya
tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kukutanisha timu nje ya
wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
AZAM WAICHAPA MBILI COASTAL UNION
![]() |
Bocco 'Adebayor' anasafiri |
MABAO mawili
ya John Raphael Bocco ‘Adebayor’ katika dakika za 15 na 44, leo yameipa Azam FC
ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa kirafiki
kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC, Septemba 11, mwaka huu,
Uwanja wa Chamazi.
Bocco
alikuwa mwiba mchungu kweli leo kwa safu ya ulinzi ya Coastal, kwani pamoja
kufunga mawili, lakini alikosa mabao matatu ya wazi mno. Abdulhalim Humud
alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 32 kwa rafu na lugha
chafu.
Hiyo ni
mechi ya tano Coastal inafungwa kati ya sita za kujipima nguvu ilizocheza kabla
ya jana kufungwa 2-1 na Yanga, awali ilifungwa 3-2 na Bandari mjini Mombassa,
baadaye 2-0 Tanga, ilifungwa 2-1 na Polisi mjini Morogoro na yenyewe iliifunga
JKT Oljoro 1-0.
Kwa Azam hii
ni mechi ya tatu mfululizo wanashinda, awali waliifunga 1-0 Prisons ya Mbeya na
Transit Camp 8-0.
Azam
inatarajiwa kuivaa Simba katika mechi ya Ngao ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa
kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Septemba 11, mwaka huu, Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa ni mchezo wake wa kwanza katika historia ya Ngao
hiyo.
Kihistoria
hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili
kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na
Yanga.
Mtibwa
ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na
kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado
inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager,
ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
Katika mechi
hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga
tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao
ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga Yanga mabao
2-0.
Ikumbukwe
mara ya mwisho Simba SC ilipokutana na Azam FC, katika Robo Fainali ya Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mwezi uliopita Dar es Salaam,
ilifungwa mabao 3-1, yote yakifungwa na Bocco na lile la kufutia machozi kwa
wekundu hao Msimbazi liliwekwa kimiani na beki mahiri Shomari Kapombe,
aliyemajeruhi kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment