
Katika mchezo huo ulioashilia kufunguliwa kwa msimu mpya wa ligi nchini Azam FC waliandika goli lakwanza katika dakika ya 5 kupitia kwa John Raphael Bocco kabla ya Kipre Hreman Tchetche kuifungia Azam goli la pili katika dakika ya 35 akiunga pasi ya John Bocco.
Wakati timu zikijiandaa kwenda mapumziko Simba SC walipo pata goli lao la kwanza kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Daniel Akuffo baada ya Said Moradi kuushika mpira katika eneo la hatari, na kuipeleka Simba mapumziko wakiwa nyuma kwa goli moja.
Kipindi cha pili Simba SC walifanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia kwa Emmanul Okwi na kisha Mwinyi Kazimoto kukamilisha magoli ya Simba SC na kutwaa Ngao hiyo ya jamii, baada ya kuitwaa mwaka jana katika mchezo ulio wakutanisha dhidi ya mpinzani wake wa jadi Yanga.
0 comments:
Post a Comment