Shirikishi la ngumi Tanzania (BFT)limeandaa mashindano ya ngumi ya ubingwa wa
Taifa 2012 yatakayofanyika kuanzia jumatatu ya tarehe 17-22/09/2012 uwanja wa
ndani wa taifa (indoor stadium) kila siku kuanzia saa 9.00 alasiri.
Awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 15/09/
2012 lakini kutokana na uwanja wa ndani wa taifa kuwa na shughuri nyingine ya
kimichezo ya ligi ya mpira wa kikapu,sasa mashindano hayo yataanza kutimua
vumbi kuanzia tarehe 17/09/2012.
Lengo la mashindano hayo ni kupata timu ya taifa ya ngumi yenye sura ya
kitaifa ,itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania bara.ili kuanza maandalizi ya
mapema na ya uhakika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola
2014,mashindano ya Afrika 2015,mashindano ya olimpiki 2016,ubingwa wa dunia
na mashindano mbalimbali tutayopata mwaliko kwa ajili ya kuwakilisha taifa.
Hadi leo jumla ya mikoa kumi na nane (18) imethibitisha kuja kushiriki katika
mashindano hayo,mikoa hiyo ni mikoa ya kimichezo ya Temeke,Kinondoni
na Ilala.Mingine ni Ngome ya JWTZ,JKT,Magereza na Polisi.Mingine ni
Pwani,Morogoro,Mbeya,Ruvuma,Dodoma,Kigoma,na Bukoba.mikoa mingine ni
Tanga,Arusha ,Tabora na Mwanza.
Uongozi wa BFT licha ya kutopata udhamini wa uhakika wa kufanikisha
mashindano haya,kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumejipanga vema
kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha hali ya juu ili kufikia
lengo la kupata timu ya taifa kwa wakati kwa maandalizi ya mapema.mashindano
hayo yana takiwa kufanyika kwa bajeti ya milioni ishirini na sita (26,000,000/=).
Sasa Mabadiliko ya ratiba ya mashindano itakuwa kama ifuatavyo:-
TUKIO
Timu zote kuwasili dare s salaam.
Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa wa ndani.
Zoezi la draw na bye na ratiba ya mashindano.
Semina kwa waamuzi,timu manaja,makocha kwa
ajili ya kupatiwa kanuni na sheria za mashindano.
18/09/2012 1.00-2.00 Asb Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa wa ndani.
8.00-2.00 Usk Gwaride la ufunguzi na kuanza mashindano hatua
ya mtoano
19/09/2012 1.00-2.00 Asb Kupima uzito na afya
9.00-2.00 Usk Mashindano kuendelea hatua ya mtoano
20/09/2012 1.00-2.00 Asb Kupima uzito na afya
9.00-2.00 Usk Mashindano kuendelea kwa hatua ya robo fainali
21/09/2012 1.00-2.00 Asb Kupima uzito
2.30-8.45Mch Mkutano mkuu wa BFT(indoor stadium)
9.00-2.00 Usk Mashindano kuendelea hatua ya nusu fainali
22/09/2012 1.00-2.00 Asb Kupima uzito na afya.
8.00-2.00 Usk Gwaride la kufunga na kuendelea kwa
mashindano hatua ya fainali.
23/09/2012
Timu zote kuondoka
Aidha ajenda za mkutano mkuu wa wanachama wa bft ni mbili tuambazo ni
kupitia na kupitisha rasmu ya katiba ya BFT na maandalizi ya uchaguzi wa BFT wa
kuwapata viongozi makiniwa kuongoza BFT kwa kipindi cha miaka mine kuanzia
marchi 2013 kwa mujibu wa katiba .
TAREHE
MUDA
16/09/2012
17/09/20123 1.00-4.00 Asb
4.00-5.00 Asb
5.00-7.00 Mch
Makore Mashaga
Katibu Mkuu BFT.,
Mob:-0713/0784/0763/0773 -58 88 18
Email:- mashagam@yahoo.om
0 comments:
Post a Comment