MSHAMBULIAJI WA SIMBA SC AONGOZA MAANGAMIZI YA ABAJALO KWA TRANS CAMP


Mshambuliaji wa zamani wa kikosi cha pili cha Simba SC Ramadhani Kipalamoto amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja katika michuano ya Azam Sport Federation Cup inayoendela nchini.

Ramadhani Kipalamoto kwa sasa anacheza katika timu ya Abajalo ya Sinza jijini Dar es salaam na leo ameiongoza timu yake katika utoaji wa kichapo cha goli 5-1 kwa Trans camp ya jijini Dar es salaam, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo ulio tumika kufungua rasmi michuano ya Azam Sport Federation Cup (ASFC), Abajalo waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 4 kupitia kwa Ramadhani Kipalamoto.

Kuingia kwa goli hilo kuliongeza ladha ya mchezo ambapo kila timu ilicheza kusaka goli huku Abajalo wakifanikwa katika dhamira hiyo kupitia kwa Ramadhani Kipalamoto katika dakika ya 11 ya mchezo.

Kuingia kwa goli hilo kulipelekea Trans camp kucheza kwa taadhari kubwa huku Abajalo wakitawala vyema eneo la kati la uwanja.

Katika dakika ya 40 Sued Mohammed aliiandikia Abajalo goli la tatu kabla ya Ramadhan Kipalamoto kuifungia goli la 4 katika dakika ya 42 na kupelekea timu kwenda mapumziko Abajalo wakiwa mbel kwa goli 4-0.

Kipindi cha pili Trans camp waliionekana wakijihami wasifungwa goli nyingi huku wakipleka mashambulizi yao ya ksuhtukiza kwa kasi wakati Abajalo wakijaribu kuupoza mchezo.

Katika dakika ya 59 Ramadhani Kipalamoto alihitimisha kalamu ya magoli kwa Abajalo kabla ya Vanas Mgili kuifungia goli pekee Trans camp katika dakika ya 84 ya mchezo na kupelekea mchezo kumalizika kwa Abajalo kushinda goli 5-1.

Kwa matokeo hayo Abajalo wamefanikiwa kutinga hatua ya pili ya michuano hiyo ambapo anatarajiwa kukutana na Abajalo katika mchezo huo unaotazamiwa kuchezwa katika mwezi wa 12 mwaka huu..

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.