PAMBA SC WATINGA HATUA YA PILI KOMBE LA AZAM


Timu ya Pamba SC ya jijini Mwanza wamefanikiwa kutinga hatua ya pili ya kombe la Azam Sport Federation baada ya leo kuwafunga Buliyambuli ya Shinyanga.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba ulishuhudia Buliyambuli wakimaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao kupewa kadi nyekundu katika dakika ya 89 ya mchezo.

Pamba SC walijihakikishia ushindi katika dakika ya 27 kupitia kwa Wiliam John goli lililodumu kwa dakika zote 90.

Kwa matokeo hayo Pamba SC ya Mwanza imefanikiwa kutinga hatua hiyo ya pili ya michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika mwezi wa 12 ikihusisha timu za ligi daraja la kwanza na timu zilizo pata ushindi katika raundi hii ya kwanza inayoendelea.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.