simba

JEBA ATIBUA MPAMBANO WA SIMBA NA YANGA, MTIBWA WATANGULIA FAINALI


Goli la kiungo ambaye soka lake amanusura likatishwa na Azam FC baada ya kudai ana matatizo ambayo yangemletea matatizo kama angeendelea kucheza mpira wakati anaitumikia Azam FC Ibrahim Rajab Jeba limeondosha fainali ya Simba na yanga katika michuano ya Mapinduzi cup baada ya kuisambaratisha Simba SC.

Katika mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa katika uwanja wa Amani mchezo ulianza taratibu kila mmoja akijaribu kujkihami na kuweka chini mpira.

Mpaka dakika 15 za kwanza zinaktika hakuna kipa aliyokuwa amepata kuokoa mpira wowote mkali langoni mwao, kitendo kilichotokana na mchezo muda mwingi kuchezwa eneo la kati ya uwanja.

Mtibwa sugar ndio waliokuwa wa mwanzo kufika langoni mwa wapinzani wao lakini walishindwa kutumia nafasi walizo tengeneza wakati simba sc wakikosa mbinu ya kupenya ukuta wa Mtibwa sugar.

Dakika ya 45 shuti kali la Ramadhani Shiiza Kichuya linashindwa kudakwa na mlinda lango wa Simba Peter Manyika na unamkuta Ibrahim Jeba na kuindikia Mtibwa goli la kuongoza na kupeleka mchezo huo mapumziko Mtibwa sugar wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili Simba SC walianza kwa kufanya mabadiliko ya kumuingiza Ibrahim Ajibu, Brian Majegwa na Said Ndemla kuchukuwa nafasi ya Awadhi Juma, Nimubona na Mussa Mgosi.

Mabadioliko hayo yalirejesha kujiamini kwa simba sc katika eneo la kati na kujaribu kutengeneza nafasi kadha ambazo walishindwa kuzitumia na kupelekea mchezo kumalizika kwa Mtibwa sugar kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na kutinga fainali.

Nusu Fainali ya pili inachezwa leo usiku kati ya yanga na URA huku mchezo wa fainali ukitarajiwa kuchezwa siku ya jumanne januari 12.


About kj

0 comments:

Powered by Blogger.