CHAMA cha Mpira wa Kikapu Dar es Salaam (BD), kinahitaji zaidi ya Sh. milioni 44 kwa ajili ya kuzisafirisha timu zake kushiriki mashindano ya majiji ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Mei 24 jijini Nairobi, Kenya.
Akizungumza na gazeti hili jana, Rais wa BD, Mwenze Kabinda alisema Jiji la Dar es Salaam mwaka huu linatakiwa kupeleka timu mbili – wanawake na wanaume.
Kabinda alisema fedha hizo wanazohitaji ni kupitia kwa wadhamini na wadau mbalimbali. Fedha hizo zitatumika kulipia usafiri, posho za wachezaji na vifaa vya michezo.
"Tayari kocha wa timu ya mkoa ameanza kuita wachezaji watakaounda kikosi kitakachokwenda kuwakilisha jiji letu.”
Aliongeza: “Tumeanza mapema maandalizi kwa sababu tunataka kwenda kufanya vizuri kwenye michuano hii."
Aliongeza kuwa BD pia imeyataka majiji ya Arusha, Tanga, Mwanza na Mbeya kuwandaa timu zao mapema.
Chanzo: Nipashe
0 comments:
Post a Comment