ASFC

KALLY ONGALA AANZA KIBARUA CHAKE KWA KICHAPO TOKA KWA JKT MLALE


Aliyewahi kuwa mchezaji wa yanga na Azam FC na kuwa kocha msaidizi wa Azam FC Kally Ongala ameeanza kibarua chake cha kukionoa kikosi cha Majimaji FC ya mjini Songea kwa kichapo toka kwa JKT Mlale.

Majimaji na JKT Mlale jana jioni walikutana katika uwanja wa Majimaji katika mchezo wa raundi ya tatu ya kombe la TFF linalo zaminia na Azam Sports na kushuhudia JKT Mlale wakiibuka na ushindi wa goli 2-1.

Ongala aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa Majimaji hivi karibuni kuchukuwa nafasi ya kocha Mzungu aliyejiuzuru baada ya timu hiyo kuwa na matokeo yasiyo ridhisha.

Kwa kichapo hicho walichopokea Majimaji kinawaondoa katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho la TFF ambapo bingwa wake atashiriki michuano ya shirikisho ya CAF hapo mwakani.

Michezo mingine ya raundi hiyo ya tatu inataraji kuchezwa januari 23 hadi januari 27 huku raundi ya nne itachezwa katika mwezi wa pili mwaka huu.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.