zanzibar

URA WATAMBA KULIPELEKA KOMBE LA MAPINDUZI UGANDA


UONGOZI wa timu ya Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA), umesema kuwa nia na madhumuni yao ni kuhakikisha wanatwaa taji la Mapinduzi katika mchezo wa fainali utakaofanyika kesho kwenye Uwanja wa Amaan dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa viongozi wa timu hiyo, Mwanjuzi Fresrick alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali, ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Yanga.


Frederick alisema kuwa hatua hiyo waliyofikia inaonesha wazi kuwa azma yao ni kuondoka na kombe hilo baada ya wachezaji wao kuonesha kiwango kizuri.

Alisema kuwa mchezo wao na Yanga wa nusu fainali ulikuwa mgumu lakini makosa yaliyofanywa na walinzi wa Yanga ndio wali yoyatumia wachezaji wake na kuweza kusawazisha bao la mapema lililofungwa na Yanga.

“Tunashukuru kufikia hatua hii na kwa uwezo wa Mungu Kombe lazima liende nyumbani Uganda”, alisema Fredrick.

Hatahivyo, alisema kuwa wachezaji wake walistahili kufika fainali kutokana na kiwango kizuri walichokionesha katika michezo yake yote.

URA ilipangwa katika kundi B katika michuano hiyo lililokuwa na timu za Simba, Jamhuri na JKU na kufikia hatua ya nusu fainali kwa kushika nafasi ya pili katika kundi hilo kwa kuwa na pointi sita wakati Simba iliotolewa na Mtibwa katika nusu fainali iliongoza kundi hilo kwa kuwa na pointi saba.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.