yanga

YANGA YAIFUATA SIMBA SC, YATOLEWA NA URA KWA MIKWAJU YA PENATI


Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga wanataraji kupata boti moja kesho na wapinzani wao Simba sc baada ya kuubali kichapo cha penati 4-3 mbele ya wakata ushuru wa Uganda URA na kupelekea fainali kukutanisha URA na Mtibwa sugar.

Katika mchezo huo wa pili wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi, Yanga SC walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Amisi Tambwe aliyefunga katika dakika ya 13 akimalizia mpira uliotema na kipa wa URA baada ya kicha cha Saimon Msuva.

URA walisawazisha goli hilo katika dakika ya 75 kupitia kwa Peter Lwisa na kupelekea mchezo huo kuamuliwa na mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kumalika wakiwa sare ya goli 1-1.

Yanga SC walitakiwa kumaliza mchezo toka kipindi cha kwanza baada ya kupoteza nafasi mbili za kujipatia goli huku wakicheza soka safi tofauti na kipindi cha pili, ambapo kadri ya dakika zilivyokuwa zinasogea URA ndivyo walivyokuwa wanachukuwa mchezo katika utawala wao.

Katika hatua ya penati Yanga walikosa penati mbili zilizo pigwa na Geofrey Mwashiuya na Malim Busungu wakati URA wakipoteza penati moja iliyopigwa na Sam Ekito.

Waliopata penati za yanga ni Kelvin Yondani, Deogratus Munish na Saimon Msuva wakati URA walikuwa ni Jean Kulaba, Said Kyenune, Deogratius Othieno na Brian Mwete.

Kwa matoeko hayo URA itakutana na Mtibwa sugar januari 13 mwaka huu katika uwanja wa Amani katika mchezo wa fainali ambapo hapo awali ulipangwa kuchezwa januari 12 lakini umesegezwa mbele kwa siku moja.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.