Mchangani

Lindi, Arusha watinga robo kili

aamsuni:

Hatua ya makundi ya kili taifa cup 2011 ilifikia tamati jana katika mikoa sita ya Lindi, Mbeya, Tabora, Morogoro, Kilimanjaro na Mwanza, huku timu nane kuelekea mkoani Arusha kwa ajili ya Robo fainali na fainali.
Timu zilizopita katika hatua ya makundi ni Mwanza katika kituo cha Mwanza, Arusha katika kituo cha Kilimanjaro, Ilala katika kituo cha Morogoro, Singinda kutoka Tabora, Mbeya katika kituo cha Mbeya na Ruvuma iliyokuwa Lindi.Timu ya mkoa wa Kagera iliyokuwa katika kituo cha Mwanza pamoja na timu ya taifa chini ya miaka 23 iliyokuwa Kilimanjaro wamepita kama best losser.
Mechi za robo fainali zitapigwa tarehe 22 na 23 mei huku nusu ikichezwa tarehe 24 na 25 mei na fainali kupigwa mei 28 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

MATOKEO YA MICHEZO YA JANA.
Arusha 1 - 1 U23 Tanzania, wafungaji: Arusha, Abdallah Juma, u23 Tanzania, Amour Suleiman
Tanga 1 - 0 Kilimanjaro, mfungaji: Juma Mwinyimvua
Ilala 1 - 0 Manyara, mfungaji: Omari Matuta
Morogoro 1 - 0 Pwani, mfungaji: Hussein Javu
Kagera 3 - 0 Shinyanga, wafungaji: Ibrahim Hassan, Shamte Adilo na Juma Nade
Mwanza 2 - 1 Mara, wafungaji: Mwanza, Jerry Tegete 2, Mara, Juma Magora
Singinda 1 - 0 Kigoma, mfungaji: Selemani Msengi
Mbeya 2 - 0 Rukwa, wafungaji: Said Mtupa na Gaudience Mwaikimba

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.