TFF

NGORONGORO KUWAKABILI MOROCCO WIKIEND HII, STARS KUELEKEA ALGERIA


Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco na Msumbuji kabla ya kuwavaa DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana (AFCON U20).
Ngorogoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Vijana ya Morocco Jumamosi Machi 17, 2018 na dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana Msumbiji Jumatano Machi 21, 2018 michezo yote ikichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20, Ngorogoro Heroes itacheza dhidi ya DR Congo Machi 31 katika uwanja wa Taifa na mchezo wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili jijini Kinshansha Congo DR.

Ngorongoro Heroes imeingia kambini katika Hoteli ya Ndege Beach iliyopo Mbweni ambapo inajiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 20.


Wakati huo Taifa Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki katika kalenda ya FIFA inayoanza Machi 19 – 27, 2018 dhidi ya timu za Taifa za Algeria na DR Congo.

Stars itasafiri kuelekea jijini Algiers kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Algeria Machi 22, 2018 na baada ya mchezo huo dhidi ya Algeria, Taifa Stars itarejea nyumbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DR Machi 27, 208 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.