ZGPL

KVZ NA MAFUNZO HAKUNA MBABE - LIGI KUU ZANZIBAR


Ligi Kuu Soka ya Zanzibar hatua ya 8 Bora imeendelea tena leo kwenye dimba la Aman wakati wa saa 10 za jioni kwa Mafunzo kugawana alama moja moja na KVZ baada ya kwenda sare ya bao 1 kwa 1.

Mafunzo walikuwa wa kwanza kuanza kuliona lango la KVZ ndan ya dakika ya 19 kupitia Jaku Joma baada ya kumalizia pasi safi aliowekewa na Abdulaziz Makame. Dakika ya 74 Jaku Joma wa Mafunzo akatolewa nje kwa kuoneshwa kadi nyekundu. Bao la kusawazisha la KVZ limefungwa na Suleiman Hassan “Kede” dakika ya 79. Hadi mwisho wa mchezo huo Mafunzo 1 na KVZ 1.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho JKU dhidi ya Zimamoto katika uwanja wa Amani na African Kivumbi dhidi ya Chipukizi katika dimba la FFU Finya.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.