VPL

YANGA YAICHAPA STAND UNITED, YAIKAMATA SIMBA SC


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya vodacom Tanzania Bara Yanga wamefanikiwa kuwafikia Simba SC, baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 3-1 mbele ya Stand united katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya vodacom/

Yanga SC leo walikuwa wanacheza mchezo wao wa 21 wa ligi kuu ya vodacom, ambapo baada ya kushinda wamefikisha pointi 46 sawa na Sima SC waliocheza michezo 20 ya ligi kuu ya vodacom.

Katika mchezo huo wa leo Yanga walianza kuandika goli la kwanza kupitia kwa Yusuph Mhilu katika dakika ya 6, kabla ya Ibrahim Ajibu kutumia vyema pasi ya Naka Edward kwa kuiandikia yanga goli la pili katika dakika ya 12.

Mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania Bara walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Katika dakiak ya 84 Stand united walifanikiwa kuandika goli la kufutia machozi kupitia kwa Tariq Seif  kabla ya Obrey Chirwa kuindika Yanga Sc goli la tatu katika dakika ya 86.

MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM BAADA YA MCHEZO WA LEO


About kj

0 comments:

Powered by Blogger.