simba

BOCCO AIMALIZA SIMBA TAIFA


Goli la nahodha wa Azam Azam FC John Raphael Bocco limetosha kuipatia pointi tatu muhimu Azam FC mbele ya Simba SC katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa hii leo.

Katika mchezo wa leo wa ligi kuu ya vodacom ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana, huku pande zote mbili zikishambuliana kwa zamu.

Katika kipindi cha pili kocha wa Azam FC, Iddi Nassoro Chechealifanya mabadiliko ya kumtoa Ramadhani Singano na kuingia Yahya Muhammed, huku Kocha wa Simba Joseph Omog akimuingiza Ibrahim Ajib.

Mabadiliko hayo yalipelekea muda mwingi Simba Sc kuwa langoni kwa Azam FC, wakati Azam wakitumia mashambulizi ya kushtukiza na mnamo dakika ya 70 John Bocco aliiandikia Azam FC goli la ushindi.

Kuingia kwa goli la Bocco klipoteza utulivu kwa Simba Sc na kama Azam FC wangekuwa makini ndani ya dakika 5 baada ya kufunga goli walikuwa na uwezo wakupata goli la pili, hadi dakika 90 zinamalizika Azam FC walikuwa mbele kwa goli 1-0.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.