aamsuni:
Baada ya sakata la Mbwana Samata kukosa jipya magazeti wame mgeukia mshambuliaji mahiri nchini kwa sasa Mrisho Khalfan Ngassa, baada ya vichwa vya habari kutawalwa na jina lake.
Ni jambo la kawaida kwa wachezaji kuhusishwa katika usajili kila kipindi cha usajili unapofika. Wakati ligi kuu inakimbilia kuisha taarifa za Ngassa kujiunga na yanga zilipata kasi lakini kuibuka kwa Mbwana Samatta kwenda TP Mazembe ilizima taarifa ya Ngassa kwa kiasi fulani.
Jana kuna magazeti kadhaa yaliripoti yanga imesha wasilisha barua kwa uongozi wa Azam kwa lengo la kufanikisha kumnasa nyota huyo wa Azam fc.
Hii leo kuna gazeti limeripoti kwa kumnukuu Ngassa mwenyewe kuwa, hana furaha ndani ya Azam fc kwa kuwa wana msema ana mapenzi na Yanga. Hivyo angependa kuondoka Azam fc kabla ya kumkuta yaliyo mkuta Amir Maftah pale Yanga.
Kama lisaa limepita hivi klabu ya Azam imetangaza kupitia ukurasa wake wa facebook kwa kusema "Azam FC haiwezi taja dau la kumuuza Ngasa kwa kuwa HAUZWI, kwa klabu za ndani isipokuwa nje ya nchi. Azam FC inawataka Yanga waache kuzungumza na Ngasa. Ngasa siyo mchezaji wao na wala siyo mchezaji huru, Ngasa anamkataba na Azam FC. ambao AzamFC haina nia ya kuuvunja isipokuwa kuuboresha," maneno ndani ya ukurasa wa Azam fc.
Katika harakati ya kujibu hoja ya mmoja ya mchangiaji katika habari hiyo, aliyepewa jukumu la kuendesha ukurasa huo alisema Ngassa ameshazungumza na viongozi wake wa Azam fc na kusema hataki kuondoka.

0 comments:
Post a Comment