ngumi

LULU AJIGAMBA KUMCHAKAZA FATUMA

BONDIA Lulu Kayage yupo katika maandalizi kwa ajili ya mpambano wake na Fatuma Omari utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Friends Corner, jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mpambano huo Kayage alisema kuwa yeye anafanya mazoezi mwaka mzima hata kama hana mchezo hivyo yupo fiti wakati wowote kucheza mpambano huo, kwani ndiye anatarajia kuwa bingwa kwa upande wa wanawake.

“Mimi nafanya mazoezi kipindi chote hivyo nipo tayari kupambana kwani natarajia nitakuwa bingwa kwa wanawake,” alijigamba Lulu.

Pia amewataka wanawake wanaoweza kuhimili vishindo vya mchezo wa masumbwi wajitokeze ili kuleta changamoto ya mchezo huo unaopendwa na watu wengi duniani.

Lulu alijigamba kuwa anaiga staili ya Leila Ali ambaye alikuwa bingwa wa mchezo wa masumbwi duniani ambaye kwa sasa amestaafu hivyo anataka afuate nyayo zake.

Mpambano huo utasindikizwa na mpambano wa mabondia Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani na wameomba mashabiki wajitokeze kuwaunga mkono na kuwatia moyo.

CHANZO: HABARI LEO

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.