SIMBA imepangwa kufungua pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi
kwa kucheza na AFC Leopards ya Kenya Januari Mosi wakati Yanga
wakishuka dimbani siku inayofuata kuikabili Tusker FC.
Msemaji wa Kamati ya Michuano ya Kombe la
Mapinduzi, Farouk Karim alisema, pambano la Simba na Leopards
litafanyika kwenye Uwanja wa Amani saa 2 usiku na litatanguliwa na mechi
kati ya wenyeji KMKM na KCC ya Uganda litakalopigwa saa 10 jioni kwenye
uwanja huohuo.
Katika michuano iliyopita Simba waliishia nusu
fainali baada ya kuondolewa na Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada
ya mechi kumalizika kwa sare ya 2-2 hata baada ya kuongezwa dakika 30.
Nao mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga
yenyewe haikushikiri michuano iliyopita kutokana na kuwa katika ziara ya
mechi za kirafiki nchini Uturuki lakini mwaka huu imethibitisha
ushiriki wao.
Yanga itashuka uwanjani Januari 2 kuivaa Tusker ya
Kenya mchezo utakaochezwa saa 2 usiku kwenye Uwanja wa Amani na
utatanguliwa na mchezo kati ya Azam na Kombaini ya Unguja utakaochezwa
saa 10 jioni.
Pia kutakuwa na mechi nyingine Januri 2
zitakazofanyika kwenye Uwanja wa Gombani Pemba kati ya URA ya Uganda
itakayoikabili Chuoni majira ya saa 8 mchana na baadaye itafuatiwa na
mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Kombaini ya Pemba utakaofanyiak saa
10 jioni.
Farouk alisema robo fainali ya michuano hiyo
itafanyika Januari 8, wakati nusu fainali itafanyika Januri 10 na
fainali Januari 13.
Alisema, mechi zote za hatua ya makundi na robo
fainali zitafanyika kwenye viwanja wa Gombani Pemba na Amani Unguja,
wakati nusu fainali na fainali zitapigwa kwenye Uwanja wa Amani.
0 comments:
Post a Comment