Kocha Kerr aliambia simbasports.co.tz “huu utakuwa ni mchezo wetu wa kwanza baada ya ligi kusimama kwa muda mfupi, ni mchezo ambao nategemea kuwa wa ushindani mkubwa sana ijapokuwa kwa maandalizi ambayo kikosi changu kimeyafanya mpaka sasa mashabiki na wapenzi wa Simba waje kwa wingi siku hiyo uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuishangilia timu yao katika kuchukua ushindi wa mchezo huo”.
Nina imani kubwa sana ya kushinda katika mchezo huo, hivyo wapenzi wote wa Simba waje kwa wingi katika kuishangilia timu yao, najua Azam FC ni moja ya timu kubwa sana na itakuwa imejipanga vya kutosha kukabiliana nasi ila siku ya Jumamosi nataka wachezaji wangu waoneshe kuwa matokeo tuliyoyapata kwenye mechi yetu ya mwisho dhdi ya Majimaji ambapo tulishinda 6 -1 hayakuwa ya kubahatisha na hivyo tutaendeleza moto tuliokwisha uanza, aliongezea Kocha Kerr.
0 comments:
Post a Comment