aamsuni
Dar es salaam, Chamazi.
Katika uwanja wa Chamazi unaomilikiwa na klabu ya azam fc ulioko nnje ya jiji la Dar es salaam kulikuwa na mtanange baina ya Azam fc na Vijana stars mchezo uliomalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.
Ikiwa ndio mechi ya kwanza kuchezwa katika uwanja huo wa chamazi, na ni mechi ya kwanza ya kirafiki kwa timu ya taifa ya u 23 inayojiaoda kuikabili cameroun apo machi 27 nchini cameroun.
Timu ya vijana stars iliyopo chini ya kocha Julio walipata goli la kuongoza katika dakika 28, na azam fc kuja kulisawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Redondo.
Dar es salaam, Uhuru.
Katika dimba la uhuru kulikuwa na mtanange wa ligi kuu ya vodacom (VPL) ambapo ulikwisha kwa mwenyeji Africa lyon kutoka kifua mbele kwa goli moja bila. Africa lyon iliyoko katika nafasi za kati katika msimamo wa ligi kuu ili wakarabisha vijana kutoka Mwanza Toto Africa.
Morogoro,
Mtibwa sugar ilikuwa inawakabili timu ya Ruvu shooting ya Pwani mchezo uliokwisha kwa sare ya goli moja kwa moja. Kutokana na sare hiyo Mtibwa sugar imepoteza matumaini ya kushika nafasi ya tatu inayoshikiliwa na Azam fc kwa sasa. Wakati huo huo Ruvu shooting wako kwenye hatari ya kushuka daraja endapo atashindwa kuzichanga karata zake katika michezo miwili iliyo salia.
Dodoma.
Katika uwanja wa jamhuri mkoani Dodoma, timu ya polisi Dodoma imeiteremsha daraja rasmi timu ya AFC ya Arusha baada ya kushinda magoli mawili kwa bila.AFC iliyokalia nafasi ya mwisho tangu ligi inaanza jana ilishuka daraja rasmi kwa kutoweza kumteremsha Ruvu shooting mwenye point 17 ambazo AFC inaweza kuzifikisha ila uwiano wa magoli ndio unao mwiweka chini. AFC inatofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa -28 huku Ruvu shooting akiwa -8.
Songea.
Jahazi la majimaji ya songea limezidi kuzama japo bado wanamatumaini ya kubakia endapo atashinda mechi zake mbili huku Ruvu shooting akipoteza.Mchezo wa jana uliochezwa katika uwanja wa Majimaji ulishuhudia mgeni Kagera sugar aki mkirimu mwenyeji wake magoli mawili kwa moja. Kutokana na ushindi huo Kagera sugar wamemteremsha nafasi moja mtibwa sugar na wao kukalia nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu vpl
0 comments:
Post a Comment