yanga

Yanga yawapima tena TFF


Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga wameiweka tena katika mtego shirikisho la soka nchini TFF kufuatia kumtumia beki Nadir Haroub 'Cannavaro' katika mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi.

Nadir alionyeshwa moja kwa moja Kadi Nyekundu iliyotokana na vurugu katika mchezo dhidi ya Azam FC, hivyo kutakiwa kukosa michezo mitatu ya Ligi Kuu ya Vodacom, badala yake amekuwa nnje kwa michezo miwili.

Sheria za ligi kuu ya Vodacom zinaeleza kuwa ukipata kadi nyekundu baada ya kadi mbili za njano unakosa mchezo mmoja, ukipata kadi nyekundu moja kwa moja ya kimchezo unakosa michezo miwili na ukipata kadi nyekundu moja kwa moja kwa kutokana na vurugu unakosa michezo mitatu.

Kitendo hicho huenda ukapelekea Yanga kupokwa ushindi wa mchezo huo, na kuwapa Coastal ushindi na point 3.

Teyari Coastal Union wameshakata rufaa, huku kukiwa na taarifa ya Azam FC nao kupeleka rufaa yao ya kupinga kuchezeshwa kwa Nadir Haroub katika mchezo huo.

Nadir na wenzake watano toka Yanga walifungiwa na kamati ya ligi, ambapo kamati ya nidhamu ya TFF, walitengua adhabu hiyo, wakiacha zile zilizotolewa na mwamuzi wa mchezo kati ya Azam na Yanga Israel Nkongo.

"Kamati inasisitiza kwamba adhabu zilizotolewa na mwamuzi wa mchezo huo katika dakika 90 za mchezo hazitahusika na amri hii ya kusitisha utekelezaji, na wachezaji wanaohusika na adhabu hizo za mwamuzi wataendelea kutumikia adhabu zao hadi hapo watakapomaliza au pale maamuzi mengine yatakapotolewa," ili eleza taarifa ya Tibaigana iliyotolewa machi 24 mwaka huu kuwafungulia wachezaji watano wa Yanga.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.