simba

BABA UBAYA WA MWANZO KUCHOMOKA MTIBWA

Kama ilivyo ada kwa Mtibwa sugar kila msimu unapo malizika baadhi ya nyota wake waliongara katika msimu uliokwisha huchukuliwa ni timu za Simba na Yanga. Safari hii aliye fungua mlango huo ni beki Issa Rashidi 'Baba ubaya'.

Beki huyo ambaye hucheza pembeni alipatwa kuitwa na kocha Kim Poulsein katika timu ya Taifa ya Tanzania kabla ya kuachwa katika safari ya kuelekea Morocco, amekuwa nguzo muhimu kwa mtibwa sugar na sasa amejiunga na Simba sc.

Kwa mujibu wa kauli ya Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa simba Zacharia Hans Pope akiieleza blogu ya Bin Zubeiry  amesema wamemsainisha beki huyo wa Mtibwa sugar sambamba na mshambuliaji aliye kuwepo kwa mkopo JKT Ruvu akitokea Azam FC Zahoro Pazi na kipa wa Kagera Sugar Andrew Ntala.

Pope alieleza kuwa wachezaji hao watatu wamepewa mikataba ya miaka miwili kila mmoja. Huku akiongeza kuwa wamewapa mikataba wachezaji wakikosi B waliopandishwa kwenye kikosi A akiwemo Haruna Chanongwa.

Nnje ya wachezaji hao watatu simba vile vile wamemsajili kinda wa Coastal union Twaha Shekuwe "Messi" na kufanya wae wameongeza kuvu mpya nne kwa ajili ya msimu ujao.


Wakati Simba yakijili hayo Coastal union ya Tanga wao wamemuongezea mkataba kiungo wao toka Kenya Jerry Santo.


g

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.