Na
Issa Mwaluhanga
MICHUANO ya 14 ya vijana inayoandaliwa na Taasisi ya Kuibua,
Kukuza na Kuendeleza Vipaji vya Soka ya Rollingstone Multipurpose
Ateclass Foundation, imepangwa kuanza Julai 6, jijini Arusha.
Mratibu wa michuano hiyo, Willybroad Alphonce, alisema jana michuano hiyo itashirikisha vijana wa chini ya miaka 20 na 15 kutoka nchi za Uganda, Burundi, Congo (DRC), Zanzibar na Tanzania Bara.
Alizitaja timu za Tanzania ni Azam FC, Simba, Coastal Union, Ruvu Shooting, Mgambo JKT, Future Talent, Bishop Durn, Younglife na wenyeji Rollingstone.
Alisema manufaa ya michuano hiyo ni makubwa kwani ndio iliyowaibua nyota wengi kama Shabani Kado, Nadir Haroub ‘Cannavaro,’ Kigi Makassy, Amir Maftah, David Mwantobe na wengineo wanaocheza nje ya Tanzania.

0 comments:
Post a Comment