Na Ally Mohammed, Zanzibar
Ligi Kuu ya Zanzibar, maarufu Zanzibar Grand Malt
Premier
League (ZGPL) iliendelea tena hapo jana kwa michezo miwili, katika uwanja wa Amaan
mjini
Unguja, Malindi ambao wamenunua daraja kutoka kwa timu ya Miembeni SC,
waliteremka uwanjani kuivaa Bandari ambayo imepanda daraja msimu huu.
Katika
mechi hiyo Bandari wameianza vyema ligi hiyo baada ya kuchomoza na
ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Malindi mabao ya Bandari yakifungwa na
Mussa Omar katika dakika ya 31 kipindi cha kwanza bao la pili likifungwa
na Haisam Khamis dakika ya 57.
Huku bao la 3 likfungwa na Shariff
Kitwana katika dakika ya 78, na mabao ya Malindi yakifungwa na Amour
Suleiman katika dakika ya 44 na 68.
Wakati katika kisiwa cha Pemba wawakilishi wa
Zanzibar katika michuano ya kombe
la shirikisho, Jamhuri wakicheza na Duma ambayo inamilikiwa na Jeshi la
Kujenga Uchumi (JKU) wameanza vizuri baada ya kuchomoza na
ushindi wa mabao 2-0, mabao ya Jamhuri yote mawili yakifungwa na Mfaume
Shaaban
katika kila kipindi, bao la kwanza akilifunga katika dakika ya 7 ya
kipindi cha kwanza, bao la pili akifunga katika dakika ya 72.
0 comments:
Post a Comment