Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa azam fc ndani ya facebook inaeleza kuwa Humud amefuzu majaribio hayo baada ya kufanya mazoezi mara moja na kucheza mechi moja.
"Abdulhalim Gaucho Humud amefuzu majaribio Jomo Cosmos, yalikuwa majaribio ya wiki mbili (siku 14) lakini amefuzu baada ya kufanya mazoezi Mara moja na kucheza Mechi moja ambapo alikua nyota wa mchezo," ilieleza taarifa hiyo.
Humud alienda Afrika kusini mwishoni mwajuma lililopita kwa ajili ya majaribio ya wiki mbili katika timu ya Jomo cosmos inayoshiriki ligi daraja la kwanza.
Humud atarejea nchini kwa kumalizia mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom, huku akingoja makubaliano kati ya azam fc na Jomo.
Humud ambaye katika mzunguko wa pili amejikuta akingoja benchi katika kikosi cha azam fc, na endapo atafanikiwa kusajiliwa katika klabu hiyo atakuwa mtanzania wa nne kuchezea timu hiyo.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html
0 comments:
Post a Comment