zanzibar

MAMBO SI SHWARI KATI YA ZFA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

Na Ally Mohammed, Zanzibar

Chama cha soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kimemuandika Barua nzito Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk ya kutaka ufafanuzi wa kutosha juu ya hatua yake ya kuamua kumrejesha kazini Katibu Mkuu aliyesimamishwa, Kassim Haji Salum.

Katika barua hiyo iliyoandikwa tarehe 8.9.2012 ambayo nakala yake tunayo, ikisainiwa na Kaimu Rais wa ZFA, Al-haj Haji Ameir, na nakala yake kutumwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo la Zanzibar, Katibu Mtendaji Baraza la Michezo Zanzibar, Makamo wa Rais wa ZFA Unguja,Makamo wa Rais wa ZFA Pemba na Kaimu Katibu Mkuu wa ZFA kisiwani Pemba.


ZFA Taifa kupitia kwa Mwanasheria wake Abdallah Juma wamemtaka Waziri huyo amsaidie Katibu huyo kujibu hoja alizosimamishiwa badala ya kuonekana kumkingia kifua.


Katika barua hiyo imesema suala la kumsimamisha Katibu huyo halikuwa adhabu lakini pia kumtaka ajieleze si adhabu bali ni fursa sahihi si ya ki-Katiba tu lakini  pia ni haki yake ya kibinadamu kwa mujibu wa sharia ya nchi (natural justice and right to be heard) na wamefanya hivyo kwa nia ya kujenga hadhi ya afisi ya Waziri huyo na ya ZFA.

Itakumbukwa kuwa chama cha soka visiwani Zanibar (ZFA) chini ya kikao halali cha kamati Tendaji kikiongozwa na Rais wa chama hicho, Aman Ibrahim Makungu, kilichokutana tarehe mwezi uliopita kilitoa maamuzi ya Kumsimamisha Katibu Mkuu wa  ZFA, Kassim Haji Salum, huku ikitoa hoja nane ambazo alitakiwa kuzijibu.

Baadhi ya hoja hizo ni Kotokuwa na uwezo wa kutumia mitandao, kutoa matamshi ya kukidhalilisha chama hicho pamoja na kutoa siri za vikao halali vya chama hicho.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.