Ally Mohammed, Zanzibar
Timu iliyopanda daraja ya Mtende Rangers imeichapa goli 3-0 timu ya Zimamoto katika muendelezo wa Zanzibar Grand malt Premier League (ZGPL) leo katika nyasi za Amaan, mjini Unguja.
Katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na watazamaji wachache ilishuhudia mabao ya Mtende yakifungwa katika dakika ya 5 kupitia Ali Salum, bao la pili likifungwa na Ali Manzi katika dakika ya 42, wakati msumari wa mwisho ukishindiliwa na Islah Khamis katika dakika ya 77.
Ligi hiyo inatarajia kuendelea tena kesho kwa mechi moja na ya mwisho katika mzunguko wa kwanza mechi itakayochezwa katika uwanja wa Amaan, majira ya saa 10:30 jioni kwa kuzikutanisha timu za Chuoni na Mundu.
0 comments:
Post a Comment