VPL

VITA NYINGINE KATI YA KAZIMOTO NA SURE


Ni vita nyingine kati ya viungo bora katika suala la kuichezesha timu nchini Mwinyi Kazimoto na Salum Abubakari 'Sure Boy Jr' katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kesho kwa kiingilio cha Tsh 5000.

Mwinyi Kazimoto toka Simba na Sure Boy Jr toka Azam FC wanakutana katika mchezo wa kufungua msimu mpya wa ligi (mchezo wa ngao ya jamii) ambapo kiutamaduni hukutanisha bingwa wa Ligi Kuu na bingwa wa kombe la chama ama shirikisho ambalo linatarajiwa kurejeshwa katika msimu unaofunguliwa kesho.

Kutokana na kukosekana bingwa wa kombe la TFF, mchezo huo unawakutanisha bingwa wa Ligi Kuu dhidi ya mshindi wa pili wa ligi katika msimu uliopita, ambao Simba SC waliibuka bingwa na Azam FC kushika nafasi ya pili.

Michezo kati ya Azam FC na Simba SC huamuliwa na namna viungo wa timu zote mbili zilivyo amka kutokana na timu zote kutegemea eneo la kati kupika magoli yake huku wakicheza soka linalo fanana.

Azam FC inaikabili Simba SC ikiwa na kocha wao mpya ambae alishuhudia kikosi chake kikichapwa goli 3 na kikosi B cha Simba katika michuano BancABC Super8, wakati kocha wa Simba SC akiwa na kumbukumbu ya kufungwa goli 3 toka kwa Azam FC katika mchezo wa robo fainali kombe la Kagame.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.