KAMPUNI ya Airtel Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza michezo nchini ili kuleta ufanisi katika sekta hiyo.
Akizungumza kabla ya kukabidhi mipira 100 kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso, alisema uwekezaji katika michezo ni muhimu hasa kipindi hiki ambacho Tanzania inajipanga kushiriki mashindano ya kikanda na kimataifa.
“Airtel Tanzania tunakabidhi mipira 100 kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 kama sehemu ya juhudi zetu kusaidia maendeleo ya michezo.
“Tutaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha nchi inapata mabalozi wa kutuwakilisha vizuri katika mashindano ya kimataifa,” alisema.
Colaso alisema mwaka 2011 kampuni yake kwa makusudi ilianzisha Airtel Rising Stars ikiwa ni mpango wa kuvumbua na kuendeleza vipaji kwa vijana wadogo kutoka ngazi ya chini ili kuwapeleka ngazi za kimataifa.
Wakati wa hafla hiyo, mkongwe wa klabu ya Manchester United, Andy Cole, aliwataka vijana hao chini ya miaka 17, kuongeza bidii ili kutimiza ndoto zao za kucheza kwenye timu kubwa duniani.
“Nimeona vipaji vingi Tanzania. Wachezaji wanaweza kabisa kuchezea klabu kubwa kama wataongeza bidii katika mazoezi yao. Naomba nichukue nafasi hii kuwakumbusha wachezaji chini ya miaka 17, kuwa na nidhamu; si ndani tu ya uwanja bali na nje ya uwanja, kwani hiyo ndio nguzo ya mafanikio,” alisema.
Naye Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, aliishukuru Airtel Tanzania kwa juhudi zake endelevu kusaidia michezo na kutoa wito kwa kampuni nyingine kuiga mfano huo.
“Tunahitaji nguvu za pamoja kati ya sekta binafsi na umma kama kweli tunataka maendeleo katika michezo. Nawashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika michezo, niyaombe makampuni mengine yaige mfano huu katika kusaidia juhudi za serikali kuendeleza michezo,” alisema.KAMPUNI ya Airtel Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza michezo nchini ili kuleta ufanisi katika sekta hiyo.
Akizungumza kabla ya kukabidhi mipira 100 kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso, alisema uwekezaji katika michezo ni muhimu hasa kipindi hiki ambacho Tanzania inajipanga kushiriki mashindano ya kikanda na kimataifa.
“Airtel Tanzania tunakabidhi mipira 100 kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 kama sehemu ya juhudi zetu kusaidia maendeleo ya michezo.
“Tutaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha nchi inapata mabalozi wa kutuwakilisha vizuri katika mashindano ya kimataifa,” alisema.
Colaso alisema mwaka 2011 kampuni yake kwa makusudi ilianzisha Airtel Rising Stars ikiwa ni mpango wa kuvumbua na kuendeleza vipaji kwa vijana wadogo kutoka ngazi ya chini ili kuwapeleka ngazi za kimataifa.
Wakati wa hafla hiyo, mkongwe wa klabu ya Manchester United, Andy Cole, aliwataka vijana hao chini ya miaka 17, kuongeza bidii ili kutimiza ndoto zao za kucheza kwenye timu kubwa duniani.
“Nimeona vipaji vingi Tanzania. Wachezaji wanaweza kabisa kuchezea klabu kubwa kama wataongeza bidii katika mazoezi yao. Naomba nichukue nafasi hii kuwakumbusha wachezaji chini ya miaka 17, kuwa na nidhamu; si ndani tu ya uwanja bali na nje ya uwanja, kwani hiyo ndio nguzo ya mafanikio,” alisema.
Naye Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, aliishukuru Airtel Tanzania kwa juhudi zake endelevu kusaidia michezo na kutoa wito kwa kampuni nyingine kuiga mfano huo.
“Tunahitaji nguvu za pamoja kati ya sekta binafsi na umma kama kweli tunataka maendeleo katika michezo. Nawashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika michezo, niyaombe makampuni mengine yaige mfano huu katika kusaidia juhudi za serikali kuendeleza michezo,” alisema.
0 comments:
Post a Comment