CECAFA

MAPUNDA AIPELEKA KILIMANJARO STARS NUSU FAINALI



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgQzHzenHBziloc1WvhWi9dUHa8nnIEUagvgQNKzyk3lt_QDENso8y18COl0thCqm8uQPo7VUjpIZ2kkb-AaVqamME7ND5oYJLhXL9VjMPKpe-dDQsfB5xNLvxQMYHhPmU7H-YnA3HIm0M/s280/ngassa.jpg

Timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kiloimanjaro stars' leo wamefanikiwa kuwavua ubingwa wa kombe la Challenge timu ya taifa ya Uganda 'The creins' kwa mikwaju ya penati 3-2 baada ya kumaliza dakika 90 wakiwa sare ya goli 2-2.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Manispaa mjini Mombasa, Kenya Uganda walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 16 kupitia kwa Dani Sserunkuma akitumia vyema krosi ya Hamisi Kiiza.

Alikuwa Mrisho Khalfani Ngassa aliyeifungia Kilimanjaro stars goli mbili katika mchezo wa leo, akiitumia vyema pasi ya mshambuliaji wa TP Mazembe Mbwana Sammata na kuisawazishia Kili Stars katika dakika ya 18 ya mchezo.

Ngassa alifunga goli la pili katika dakika ya 38 kwa mpira wa adhabu na kuiplekea Kilimanjaro stars mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-1.

Katika kipindi cha kilimanjaro stars walipata pigo kufuatia kadi nyekundu aliyo onyeshwa kiungo wa Azam FC Salum Aboubakari 'Sure Boy' katika dakika ya 53 ya mchezo.

Katika dakika ya 73 Martin Mpugaaliisawazishia Uganda akiunganisha kona ya Godfrey Walusimbi na kupelekea dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 2-2.

Katika hatua ya mikwaju ya Penati kipa Ivo Mapunda alifanikiwa kucheza penati 2 za Uganda huku penati moja wakitoa nnje na kluwa na penati 3 walizo zikosa katika mchezo huo.

Penati za Uganda zilizo tinga kwenye nyavu za Ivo Mapunda ni za mshambul;iaji wa zamani wa Simba Emanuel Okwi na mshambuliaji wa Yanga Hamisi Kiiza.

Wakati Kilimanjaro stars wakikosa penati mbili zilizo pigwa na Mbwana Samata na Erasto Nyoni, huku zilizo tinga katika nyavu za kipa wa Uganda zikiwa zimepigwa na Athumani Iddi 'Chuji', Kelvin Yondani na Amir Kiemba.

Kikosi cha Kilimanjaro stars leo: Ivo Mapunda, Michael Aidan, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mrisho Ngassa/Athumani Iddi 80, Amri Kiemba, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Uganda; Benjamin Ochan, Nico Wadada, Muga Martin, Geoffrey Kizito/Said Kyeyune dk64, Godfrey Walusimbi, Kasaga Richard, Khalis Aucho, Mpande Joesph/Brian Majwega dk46, Daniel Sserunkuma, Hamisi Kiiza na Emmanuel Okwi.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.