simba

SIMBA WAONGEZA WIGO POINTI, AZAM WAKIAMBULIA SARE SONGEA


Vinara wa ligi kuu ya vodacom Simba SC wameongeza tofauti ya pointi kati yao na watani wao Yanga kutoka pointi moja mpaka pointi 4 baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya JKT Ruvu mchezo uliochezwa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi na kushambuliana kwa zamu Simba SC iliwabidi kungoja mpaka dakika ya 45 kuandika goli pekee la mchezo huo lililofungwa na Mzamiru Yassin, aliyemalizia krosi ya Pastori Athanas baada ya kipa wa JKT Ruvu kuanguka chini baada ya kuoka mpira.

Katika kipindi cha pili Simba SC walitengeneza nafasi nyingi ukilinganisha na kipindi cha kwanza lakini safu yake ya ushambuliaji ilishindwa kuzitumia nafasi hizo.

JKT Ruvu nao hawa kuwa nyuma katika kutengeneza nafasi, ambazo nao walishindwa kuzitumia na kupeleekea mchezo kumalizika kwa Simba SC kushinda goli 1-0.


Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja wa Majimaji mjini Songea, Azam FC wamelazimishwa sare ya goli 1-1 na wenyeji wao Majimaji.

Magoli katika mchezo huo yalifungwa na Yahay Muhammed kwa upande wa Azam FC na Kondo Alex kwa upande wa Majimaji.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.