simba

SIMBA SC YAICHAPA TATU MWADUI BOCCO AKITUPIA MOJA

Mfungaji bora wa wakati wote katika timu ya Azam FC John Raphael Bocco leo amefunaua daftari lake la magoli. ndani ya Simba SC katika ushimdi wa goli 3-0 walio upata mbele ya Mwadui FC.

Simba SC leo walikuwa wenyeji wa Mwadui FC katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam katika mwendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania bara.

Simba SC waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 7 kupitia kwa Emanuel Okwi likiwa ni goli lake la 5 msimu huu. Goli lililo wapeleka Simba SC mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Katika kipondi cha pili Emanuel Okwi ambae ni kinala wa Magoli msimu huu, aliiandikia Simba SC goli la pili likiwa ni goli lake la 6 msimu huu katika dakika ya 67 kabla ya John Bocco  kuifungia Simba SC goli la 3 likiwa la kwanza kwake toka ajiunge nao kwenye dirisha la usajili lililopita katika dakika ya 71.

Ushindi wa goli 3-0 walioupata Simba SC inawafanya wafikisha pointi 7 sawa na Azam FC na kuwafany washike nafasi ya pili wakiwa nyuma kwa pointi 2 dhidi ya vinara Mtibwa Sugar.

Katika mchezo mwingine wa VPL uliochezwa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, Mbeya City wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Njombe Mji.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.