Beki wa kushoto wa Simba aliyekuwa katika mchakato wa kutolewa kwa mkopo Juma Jabu 'JJ' amerejeshwa kundini baada ya simba kuvusha idadi ya wachezeji wakutolewa kwa mkopo.
Simba ilitaka kuwatoa kwa mkopo wachezaji saba ambapo ni kinyume na kanuni, ambazo zinaitaka klabu kutoa wachezaji wa tano kwa mkopo. Kutokana na hiyo kanuni Simba wamemrejesha Juma Jabu huku wakimuacha rasmi Meshack Abel. Meshack anatajia kwenda kufanya majaribio nnje ya nchi.
Makamu mwenyekiti, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kuwa wamemrudisha Juma Jabu na atabaki na timu kama kawaida. "Jabu amerudi kikosini na ataendelea na timu kama kawaida, lakini pia tumevunja mkataba na Meshack sasa sio mchezaji wetu tena baada ya kuomba aachwe,’’ alisema Kaburu.
Kaburu aliongeza kuwa kiungo Mohamed Banka waliye mpeleka Villa Squad wame mrekebishia mambo yake aliyo omba yafanyike na amekubali kuichezea Villa.
Katika hatua nyingine kikosi cha Simba kimeondoka jana kwenda Zanzibar bila nyota wake Haruna Moshi ‘Boban’, Salum Machaku, Salum Kanoni, Salum Kapombe walioitwa timu ya taifa, kikosi hicho kinatarajiwa kurudi Dar es Salaam Agosti 8 kwa ajili ya sherehe za siku ya Simba.

0 comments:
Post a Comment